YOUSSOU N’DOUR KUWANIA URAIS SENEGAL

January 4, 2012 at 7:41 am | Posted in Uncategorized | Leave a comment
Tags:

Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N’dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Youssou N’dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).

Hatua ya bwana Youssou N’dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.

Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.Image

DITTO APIGA REMIX YA ”NIAMINI” YA PROF JAY

December 16, 2011 at 7:45 am | Posted in Uncategorized | Leave a comment

Image

Msanii mahiri wa muziki nchini Tanzania kutoka kundi la Tanzania House Of Talents (THT) amefunguka kuwa amepiga remix kali Classic song ya nyimbo ya nyimbo iliyowahi kutamba ”Niamini” ya gwiji wa muziki Prof. Jay na anatarajiwa kuiachia hivi karibuni ikiwa ni moja ya project zake kali zinazofuata.

Ditto pia amebainisha kuwa video ya nyimbo yake inayotamba kwa sasa Tushukuru kwa yote imekamilika na ataiachia katika station mbalimbali muda wowote kuanzia sasa ambapo amesisitiza mashabiki wake kukaa tayari kwa vitu vyake vikali.

P UNIT WALAMBA BINGO

December 15, 2011 at 1:36 pm | Posted in Uncategorized | Leave a comment

Kampuni maarufu ya kompyuta duniani, inasemekana kuchagua kundi la muziki la P Unit kama wawakilishi ama uso wa bidhaa zao ndani ya Kenya

Uidhinishaji wa mpango huu utakuwa ni leo ambapo mkataba huu utasainiwa katika ofisi za kampuni hii maarufu zilizopo Upper Hill, na inasemekana kuwa utakuwa ni mkataba wa mamilioni ya shilingi kwa mujibu wa vyanzo vya habari.

Kama P-Unit wataingia katika mpango huu, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya masuala ya teknolojia ya mawasiliano na taarifa kuwatumia watu mashuhuri kama mabalozi wa bidhaa hasa katika Kenya.Image

LIl WAYNE MATATANI SA

December 14, 2011 at 12:30 pm | Posted in Uncategorized | Leave a comment

Rapa Lil Wayne a.k.a Weezy, ameripotiwa kuingia katika ugomvi na kupigana alipokuwa ziarani nchini Afrika Kusini sambamba na kundi lake la Young Money.

Weezy aliingia katika ugomvi huo baada ya kukutana na rapa mwenye swagga kama zake wa nchini humo anayejulikana kama Young Nucho katika ukumbi mmoja wa starehe ambapo uwepo wake ulionekana kumkera Weezy.

Weezy alitaka rapa huyo aondoke mahali hapo na ugomvi ukatibuka baada ya Nucho kugoma kuondoka na kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi wawili hao pamoja na wapambe wao walikoromeana hadi kufikia hatua ya Weezy kumpiga kofi Nucho. Image

Blog at WordPress.com.
Entries and comments feeds.