YOUSSOU N’DOUR KUWANIA URAIS SENEGAL

January 4, 2012 at 7:41 am | Posted in Uncategorized | Leave a comment
Tags:

Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N’dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Youssou N’dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).

Hatua ya bwana Youssou N’dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.

Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.Image

Leave a Comment »

RSS feed for comments on this post. TrackBack URI

Leave a comment

Create a free website or blog at WordPress.com.
Entries and comments feeds.